Burudani

Suma Mnazareti adai kujua mashabiki wanataka muziki upi ndio mtihani mkubwa

Suma Mnazareti anaamini kuwa mtihani mkubwa wanaokumbana nao wasanii wengi ni kujua muziki upi Watanzania wanautaka pamoja na muda gani.

Suma Mnazareti

Rapper huyo ameiambia Bongo5 kuwa hicho pia ni kitu kinachomsumbua.

“Nafikiri sasa hivi kuna aina fulani ya muziki ambao upo pia ndio maana muda mrefu ilinibidi nikae kimya. Ilikuwa inaniuma kwa sababu hata watu wananiambia ‘kwanini hutaki kuachia ngoma na unazo nyingi ndani?’ Nikawaambia kurekodi nyimbo nyingi sio kuachia ngoma nyingi kila siku kila mwezi.

“Tatizo unaachia ngoma kila siku inafika wapi? Mimi nahitaji ngoma ambayo inaweza kuingia kwenye competition na ngoma nyingi kubwa za watu . Kwahiyo naamini ujio wangu na ngoma Ndele utakuwa poa sana kwa sababu baadhi ya mastaa pamoja na presenters walioisikiliza wameikubali sana,” alisema.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents