Habari

Swissport kutoa gawio la Sh. Bilioni 1.8 kwa wanahisa wake

KAMPUNI ya Swissport inatarajia kutoa gawio la Sh. Bilioni 1.8 kwa wanachama wake baada ya kupata faida ya Sh. Bilioni 3.6 kwa mwaka 2023.

Hayo yamebainishwa jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo, Mrisho Yassin wakati wa mkutano wa 39 wa wanahisa ambao ulikuwa na agenda ya kupitisha mahesabu ya mwaka 2023 pamoja na kugawa gawio kwa wanachama wake.

Yassin anasema faida ya kampuni kwa mwaka 2023 ilikuwa Bilioni 3.6 hivyo wanahisa wa Swissport wanapewa asilimia 50 ya faida ambayo wameitengeneza kwa mwaka huo.

“Mwaka 2022 kampuni ilipata faida Bilioni 2.6 na mwaka 2023 imepata Bilioni3.6 utaona hapa faida imeongezeka na hii imechangiwa na kuongezeka kwa miruko ya ndege, idadi ya mizigo ambayo tulihudumia katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kulius Nyerere na Kilimanjaro iliongezeka hali ambayo ilisababisha kuongezeka kwa mapato yetu. Hata hivyo gharama zetu za uendeshaji hazikuongezeka,” anasema

Mmoja wa wanahisa katika kampuni ya Swissport Irene Tarimo akizungumza na waandishi wa habari

Aidha anasema kama kampuni wanania ya kutanua wigo na wanaimani siku moja wataweza kutoa huduma zao katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa Abeid Amani Karume Zanzibar, viwanja vingine hapa nchini na Afrika kwa ujumla.

“Jitihada za serikali ni kubwa katika kukuza utalii na hii imesababisha kuongezeka kwa watalii na wageni pwanaokuja Tanzania, hivyo mizigo pia imeongezeka hasa usafirishaji nje ya nchi,” anasema

Naye mwanahisa wa kampuni hiyo, Aika Shauri anasema mkutano huo umekwenda vizuri na wanashukuru kwa gawio waliolipata na wanaona kampuni hiyo inaendelea kukua.

Irene Tarimo ambaye pia ni mwanahisa wa muda mrefu wa kampuni hiyo amasema Swissport inafanya vizuri hasa ya kuwasaidia wanachama wake kuweza kujikwamua kiuchumi.

“Wale ambao wanaweza kuja kuwekeza kama Swissport inavyofanya basi wasisite wafanye hivyo ili kuweza kuwasaidia watanzania kujikwamua kiuchumi na kuondokana na umaskini,” anasema

Written by Janeth Jovin

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents