Habari

Taarifa kwa vyombo vya habari kuhusiana na tamasha la filamu la kimataifa la Zanzibar, ZIFF

Tamasha la 16 la Filamu la Kimataifa/Tamasha la Nchi za Jahazi linategemewa kuanza mjini Zanzibar tarehe 29 Juni hadi 7 Julai, 2013. ZIFF inawakaribisha sana kushiriki nasi katika siku hizi tisa za maonesho ya filamu, utamaduni, kazi za mikono na burudani, tukiwa na imani kwamba fursa hii adhimu itaweza kuwa nafasi nyingine tena katika kuenzi na kukuza Tamaduni zetu.

ZIFF Poster 2013

Dhamira kuu ni kuhakikisha ZIFF inaleta mabadiliko katika tasnia ya filamu hapa nchini, ZIFF pia imekua ikitoa ajira za muda mfupi kwa washiriki wote, kuibua vipaji na kuzitangaza kazi mbalimbali za sanaa na wasanii wa hapa nyumbani.

Kwa udhamini mkubwa kabisa wa ZUKU kwa mwaka wa pili sasa tumeweza kuwafikia watengenezaji filamu wengi wa Afrika Mashariki na kati ambako kote ZUKU wamekua wakitutangaza vyema. ZIFF itaendelea kushirikiana na ZUKU kwa miaka mingine nane wakiwa ndio wadhamini wakuu wa Tamasha.

FILAMU ZIFF 2013:

Wataayarishaji wa filamu zaidi ya 35 mahiri toka nchi mbalimbali duniani ambao filamu zao zimechaguliwa kuingia ZIFF watahudhuria Tamasha hilo na pia watatumia fursa hiyo kuongelea filamu zao na utengenezaji wa filamu kwa ujumla. Hii ni nafasi nzuri kwa watengenezaji filamu wa hapa nyumbani kuhudhuria na kupata nafasi ya kubadilishana mawazo na wenzao toka nchi mbalimbali.

Ikumbukwe zaidi ya Filamu 257 toka nchini mbali mbali ziliwasilishwa mwaka huu, lakini ni Filamu 80 zilizofanikiwa kuchaguliwa kuoneshwa na pia katika kushindania Tuzo za ZIFF. Tuzo zitolewazo katika ZIFF ni Verona, Signis, Sembene, ZUKU na Tuzo za ZIFF. Tuzo za filamu za kitanzania mwaka huu zimeshirikisha filamu 14 kutoka hapa Tanzania. Tuzo Kuu itolewayo katika ZIFF ni Golden Dhow Award (Jahazi la Dhahabu).

Pia ZUKU itatoa tuzo kwa filamu iliyotengenezwa na muongozaji wa kiafrika, imetengenzwa Afrika, imepigwa picha Afrika na pia kuwatuza msanii bora wa kiume na kike.

VIKUNDI VYA BURUDANI ZITAKAZO SINDIKIZA TAMASHA LA 16 LA FILAMU- ZIFF 2013 ni pamoja na Mrisho Mpoto na Mjomba Band, Skylight Band, Linah, Fid Q, Barnaba, Jhikoman, Baby J, Synerg, Swahili vibes, Safi theatre, Tongwa Assembly(walimu wa chuo cha saa Bagamoyo), Mkubwa na wanawe(Said Fela), kundi la Shiwe kutoka Comoro na makundi mengine mengi kutajwa hapo baadae.

JUKWAA LA WATOTO – CHILDREN PANORAMA, mwaka huu ni tofauti na miaka iliyopita, jukwaa hili litahusisha watoto toka nchi tatu za Afrika Mashariki, Uganda, Tanzania na Kenya. Jukwaa hili litatoa nafasi kwa filamu za watoto kuoneshwa katika kipindi cha Tamasha na litawafikia wanafunzi zaidi ya 1500 kutoka shule za msingi na sekondari za Zanzibar pia kutakuwa na Warsha Mafunzo (Workshop) juu ya utengenezaji wa Katuni (Animation) – Warsha hii imedhaminiwa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali – Zanzibar.

JUKWAA LA VIJIJINI – VILLAGE PANORAMA, jukwaa hili litahusisha vijiji 10 vya Unguja na 3 vya Pemba, kutakuwa na Filamu zitakazooneshwa pamoja na warsha mbalimbali za wakinamama na Watoto na Afya ya Uzazi salama.
JUKWAA LA KINAMAMA – WOMEN PANORAMA, jukwaa hili mara nyingi huambatana na jukwaa la Vijijini, Kutakuwa na Warsha juu ya wanawake na uzazi salama, Kutakuwa na Warsha juu ya unyanyasaji wa kijinsia sehemu ya kazi na Kutakuwa na Warsha juu ya wanawake, filamu na afya na litadhaminiwa na PSI/UNFPA.

MAONESHO (EXHIBITIONS) “SOKO FILAMU”, Mabanda ya maonesho mbalimbali ya kazi za sanaa za mikono na ubunifu (Made in Tanzania), wakati Tamasha SOko-Filamu hutoa fursa kwa watu kununua na kuuza kazi za mikono pamoja na kutengeneza mitandao ya kibiashara. Kutakuwa na banda Maalum la ZUKU ambalo litatumika kama sehemu maalum ya kuuza ving’amuzi lakini pia ni sehemu ya kununua kazi za wasanii (filamu).

MASHINDANO YA MBIO ZA JAHAZI (DHOW RACE) KUFANYIKA TAREHE 30 JUNE, Majahazi 10 yaitashiriki katika mashindano ya Mbio za Majahazi Baharini, ambapo mshindi atazawadiwa wa kwanza atapata 200,000, Mshindi wa pili 150,000 na Mshindi wa tatu 100,000 za Kitanzania na Mashindano haya ni kwa Udhamini Mkubwa wa Zanzibar Connection.

Mwaka huu tuna Warsha Mafunzo (Workshops) zifuatazo: –
• Watoto – Utengenezaji Katuni (Animation)
• Juigiza katika Kamera (Acting for Camera)
• Uandishi Habari za Sanaa (Arts Journalism)
• Uandishi wa Miongozo ya Filamu (Script Writing)
• Utengenezaji Filamu (Film production)
• Uandishi Chambuzi (Critical Journalism)
• Malaria & HIV- Pemba

KONGAMANO – Juni 28 hadi Juni 30, mwaka huu kutakuwa na Kongamano maalum la “Bongo Movie Symposium” litakaloendeshwa na Murdoch University kuanzia tarehe 28-30 June na litajadili kitabu kinachohusu Bongo Movie ambacho kimehaririwa na Prof Martin Mhando.

FASHION SHOW – Juni 29, Kwenye uwanja wa Mitindo Tamasha la 16 la filamu Tanzania ZIFF kutakuwa na onesho maalum la mavazi zitakalo ongozwa na Mustafa Hassanali, Farouque Abdella na Javed Jaffary mnamo tarehe 29 June.

FESTIVAL OF FESTIVALS – Juni 30 hadi Julai 6, hii huwa ni fursa ya kujitangaza kibiashara katika ZIFF na mwaka huu kutakuwa na Iran, Australia, South Africa, ZUKU na TANAPA kila siku kuanzia saa 8 mchana – 11 jioni katika Ukumbi wa Maru Maru Hotel. Ila Mwaka huu ZUKU watachukua Fursa hii kukutana na watengenezaji filamu wa kitanzania na kujadili soko la filamu Tanzania na pia kununua kazi za watengenezaji filamu wa kitanzania.

SIKU MAALUM YA FILAMU ZA KIBONGO – SWAHILI DAY – Julai 5, Filamu 14 kutoka Bongo Movie zitaoneshwa kuanzia asubuhi hadi jioni kila siku katika kumbi maalum ili kutoa nafasi kwa watu mbalimbali kuona kazi za nyumbani. Siku ya tarehe 5 ni siku maalum imetengwa kama muendelezo wa ZIFF kuonesha kujali kilicho cha kwetu, filamu za Kiswahili zitaoneshwa katika jukwaa kuu na pia kuwakaribisha wasanii mbalimbali kuhudhuria Tamasha na kupata nafasi ya kukutana na watengenezaji filamu wengine nia na madhumini ni kuzipa kipaumbele na kuenzi kazi za filamu za wasanii wa Kitanzania.

USIKU WA TUZO (AWARD NIGHT) – Julai 6, Tuzo zitatolewa kupitia Filamu 80 zinazowania Tuzo mbalimbali katika Tamasha la 16 la filamu ZIFF 2013 na MWISHO WA TAMASHA ni Julai 7
MGENI RASMI (CHIEF GUEST), mwaka huu mgeni wetu maalum atakua Tonya Lee Williams, muigizaji Muingereza ambaye amecheza tamthiliya kubwa Marekani ya The Young and the Restless na the Bold and the Beautiful, pia Tonya atafanya warsha ya uigizaji katika ZIFF.

FILAMU YA UFUNGUZI, mwaka huu filamu ya “The Reluctant Fundamentalist” kutoka kwa mtengeneza filamu maarufu na mwanzilishi wa Maisha Film Lab, MIRA NAIR ndiyo itakua filamu ya ufunguzi na filamu hii imetengenezwa nchini Marekani, India na Sweden.

WADHAMINI WETU 2013 ni: –
• Zuku –Mdhamini Mkuu
• Azam Marine
• Ethiopian Airways
• Prime Time Promotions
• GIZ
• Goethe Institute
• German Cooperation
• TMF
• Murdoch University
• Zanzibar Beach Hotel
• Zanzibar Connection
• Zanlink
• Grand Palace Hotel
• Maru Maru Hotel
• Wavuvi Restaurant
• WIOMSA
• PSI
• UNFPA
• Visual Media Institute – Iran
TUNAPENDA PIA KUTAMBUA MCHANGO WA SERIKALI YA ZANZIBAR NA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents