Habari

TAFITI: Watu wanaohangaika kulipa madeni wapo hatarini kukumbwa na magonjwa ya moyo

Je, wewe ni mmoja ya watu wanaohangaika kulipa madeni? basi ni mmoja wao ni vyema ukajitahidi kulipa madeni hayo kwani utafiti unaonesha kuwa watu wanaohangaika au kushindwa kulipa madeni wapo hatarini zaidi kukumbwa na magonjwa ya moyo ukiwemo ugonjwa wa shambulizi la moyo (Heart Attack).

Utafiti huo uliofanywa na wasomi kutoka katika chuo kikuu cha Witwatersrand cha nchini Afrika Kusini wamesema watu wengi wanaohangaika kulipa madeni wapo kwenye hatari ya kupatwa na maradhi ya moyo mara 13 ya watu wanaohangaika kutafuta kazi na wale wenye changamoto kwenye sehemu zao za kazi.

Utafiti huo uliyoongozwa na Dkt. Denishan Govender umeonesha kuwa watu wengi wenye madeni hukosa usingizi na muda mwingine hukosa amani kila wanapokumbuka madeni kitu ambacho kinawafanya wakose amani muda wote.

Dkt. Denishan Govender amesema walichukua idadi ya wagonjwa 106 wanaougua ugonjwa wa Shambulio la Moyo, ambapo wagonjwa 96 kati ya hao wamesema kuwa walikuwa wamepatwa na msongo wa mawazo kwa madeni na majukumu ya kifamilia.

Tulichogundua ni kwamba watu wengi wanapoenda hospitalini wanaulizwa vitu tofauti na madaktari kwani maswali yao utasikia unatumia sigara? au unatumia pombe au unalala muda gani? kumbe hiyo huenda isiwe sababu ya moja kwa moja.“amesema Dkt. Govender kwenye kongamano kubwa linaloandaliwa kila mwaka nchini Afrika Kusini maalumu kwa kutoa elimu ya afya ya moyo.

Wagonjwa wengi wanashauriwa kupunguza msongo wa mawazo kwa kufanya mazoezi ila fikiria kwa nini magonjwa ya moyo kama Shambulizi la Moyo hayapungui? hapa kuna sababu kama hizo za kiuchumi ambapo hata kama mgonjwa akifanya mazoezi wiki nzima bado hawezi kusahau madeni au majukumu mengine yanayohitaji fedha kuna vitu vimebadilika kwa dunia ya sasa.“amesema Dkt. Govender.

Hata hivyo, Dkt. Govender amesema kuwa watu wengi magonjwa ya moyo huwapata pale wanapoanzia utotoni lakini dalili zake huanza kuonekana kadri umri unavyozidi kuogezeka.

Kwenye utafiti huo umeonesha kuwa mabadiliko ya kiuchumi na aina ya vyakula ndio vyanzo vikubwa vya magonjwa ya moyo. Pengine kuliko hata matumizi ya sigara au pombe.

Vyanzo: Daily Mail & British Heart Foundation 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents