Habari

Tanga wazalisha panya na kuwauzia wanafunzi tsh 5000

Taasisi ya Wakala wa maabara za veterinary Tanzania mkoani Tanga ,imeanza shughuli za ufugaji panya katika taasisi hiyo.

https://www.instagram.com/tv/CCu1RmrhLQg/?igshid=syzv1ctfrkrv

Dr. OLIVA MANANGWA ni miongoni mwa watafiti wa katika taasisi hiyo ambapo Akizungumza kwa niaba ya mkuu wa ofisi hiyo mkoani Tanga amesema kwamba hivi Sasa katika kituo Chao hiko wanaendelea na mradi wa ufugaji kwa wingi panya ambapo amekiri kuwa wateja wao wakubwa ni wanafunz kutoka shule za sekondari kwaajili ya masomo ya vitendo katika maabara zao mashuleni.

Aidha katika hatua nyingine akizungumza na @bongofive ofisini kwake mtafiti huyo amegusia kuhusu homa ya mapafu kwa mifugo na huku akisema bado ni miongoni mwa magonjwa yanayosumbua mifugo mingi mkoani Tanga kwakuwa idadi kubwa ya wafugaji wananua kwa wingi dawa za homa hiyo.

Hata hivyo amewaomba wafugaji mbali mbali mkoani humo Tanga kujitokeza kuituma taasisi yao kwaajili ya ushauri namna ya ufugaji Bora wa mifugo ili waweze kuepukana na magonjwa yasio ya lazima katika mifugo yao.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents