Burudani

Tangu nianze muziki nimekuwa nikitoa hit baada ya hit – Shetta

Rapper Shetta amesema tangu aanze muziki hajawahi kutoa wimbo ulioshindwa kufanya vizuri huku ‘Shikorobo’ ikiwa ni hit ya nane.

11247567_982663195112328_390055628_n

Shetta ameiambia Bongo5 kuwa alichojipanga ni kuendelea kufanya kazi za kiwango cha juu ili asiwaangushe mashabiki wa muziki wake.

“Mashabiki wakiwa na imani na mimi ya kupata muziki mzuri mimi natakiwa kuendeleza matumani yao,” amesema. “Ukiangalia tayari nina hits 8 kwenye muziki hiyo ni dalili ya kuendeleza vitu vizuri. Sidhani kama mashabiki wana wasiwasi na mimi kwa sababu toka nimeanza sijawahi waangusha,” aliongeza.

Katika hatua nyingine, Shetta ambaye hivi karibuni aliteuliwa rasmi kuwa balozi wa Star Times, amesema anajivunia kuchukua nafasi ya marehemu Steven Kanumba.

“Mungu anasaidia sana safari yangu ya muziki inazaa matunda zaidi. Sasa hivi nimekuwa balozi wa Star Times, nimerithi nafasi ya Kanumba, so it’s official kwahiyo kuna wengi yanakuja.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents