Michezo

Tanzania yapanda juu viwango vipya vya FIFA

Katika viwango vya ubora wa Soka Duniani vinavyotolewa kila baada ya mwisho wa mwezi na FIFA leo April 6, Tanzania imepanda juu kwa nafasi 22.

Tanzania kwa sasa imefanikiwa kusogea hadi nafasi ya 135 kutoka nafasi ya 157 yaani imepanda kwa nafasi 22.

Mwezi March Tanzania imecheza mechi mbili ambazo ni dhidi ya Burundi ikashinda kwa goli 2-1 na dhidi ya Botswana iliyoshinda kwa goli 2-0.

Tanzania wakati inakutana na Burundi walikuwa katika nafasi ya 139 na imeshuka hadi nafasi ya 141 wakati Botswana ilikuwa 116 na imeshuka hadi 120.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents