Burudani

#TECNOOwnThe Stage: Upigaji kura kumchagua mshindi waanza, fainali ni Feb 7

Episode ya 12 ya TECNO Own The Stage imeruka Jumapili, January 31, na kushuhudia washiriki wakiendelea kutafuta nafasi nzuri kujiandaa na fainali ya February 7.

Fainali zitafanyika jijini Lagos ambapo mshindi atanyakua kitita cha $25,000, recording deal, na simu mpya ya TECNO Phantom 5. Katika show hiyo msanii wa Nigeria, Adekunle Gold alitumbuiza ukumbi kwa hit yake, Shade.

Kwa upande wa washiriki, Pascal alianza kwa kutumbuiza wimbo wa Kidum, Mapenzi kabla ya kumpa kijiti Shaapera aliyeimba wimbo wa Brenda Fassie, ‘Umuntu Ngumuntu Ngabuntu’.

M.I. alimsifia mnaijeria huyo akidai kuwa ingeweza hata kumwamsha marehemu Brenda kutokana makaburini. Sikin naye alitupa karata yake kwa kutumbuiza wimbo wa Miriam Makeba, ‘Soweto Blues’.

Mkenya huyo aliimbia kwa hisia sana kiasi ambacho Yemi alishindwa kuzuia machozi yake. Kwa upande wa mwakilishi wa Tanzania, Nandy, hakwenda mbali zaidi baada ya kutumbuiza wimbo wa Vanessa Mdee, Hawajui.

2016-01-31-25

Performance yake ilifunika zaidi kuliko zote kiasi cha kuunyanyua ukumbi. Kwa show yake, M.I. alitabiri kuwa Nandy atakuja kuwa bonge moja la supastaa.

2016-01-31-16
Fainali ya Jumapili itawakutanisha Nandy, Shaapera, Sikin na Pascal

Hivyo kwa sasa zoezi la kupiga kura limefunguliwa rasmi na unaweza kufanya hivyo kwa kuingia kwenye website ya shindano. Bonyeza hapa kupiga kura.

Matokeo yatatangazwa Jumapili siku ya fainali. Usikose show ya fainali itakayoruka live kupitia Africa Magic Showcase.

Usipitwe na info zote muhimu kuhusu show hii kwa kufuata akaunti za mitandao ya kijamii:
YouTube- https://www.youtube.com/channel/UCbG37SOg6yfKXnD0byZUkUA
Facebook – Tecno Own The Stage
Twitter – @tecnoowndstage
Instagram – @tecnoownthestage

Jiunge kwenye mazungumzo na kuwa huru kulike, kucomment na kushare ukipendacho Hakikisha unashare na washkaji wako kila kitu kizuri kwa kutumia hashtag, #TECNOOwnTheStage.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents