Burudani
The-Dream aondoka Def Jam Records
Baada ya kukaa kwa miaka saba, mtayarishaji wa muziki na mwandishi wa nyimbo, The-Dream ameondoka Def Jam Records.
Muimbaji huyo aliweka tangazo hilo kwa kuweka logo ya Def Jam na kuandika: I will miss this logo. It all started here! Love Everything that I achieved there, EXODUS THE-DREAM #exodusthedream.”
Akiwa na label hiyo, The Dream alitoa album tano ambazo ni pamoja na LoveHate (2007) Love vs. Money (2009) Love King (2010) Terius Nash: 1977 na IV Play ya mwaka jana.
The-Dream aliteuliwa kuwa Makamu Mkuu wa Rais wa A&R hapo Def Jam mwaka 2012 na ametengeneza nyimbo za wasanii kama Rihanna, Justin Bieber, Mariah Carey na Beyonce. “Let the New Tides bring The Things not yet seen. There’s more where those came from,” alisema.