Habari

TRA yaongeza muda wa kuhakiki TIN namba

Mamlaka ya mapato Tanzania TRA, imesogeza mbele zoezi la uhakiki wa TIN namba ya mlipa kodi kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam, kufuatia kuwepo kwa idadi kubwa ya watu wanaojitokeza kuhakiki namba zao katika kipindi hiki. Hiyo ni baada ya kutofanya hivyo miezi ya mwanzo ya zoezi hilo lililopangwa kumalizika tarehe 15 mwezi huu. Sasa litaendelea hadi Novemba 30 mwaka huu.

1-12

Akizungumzia hatua hiyo mkurugenzi wa elimu na huduma kwa mlipa kodi TRA,Richard Kayombo, amesema uhakiki wa TIN namba unawahusu wafanya biashara na wasiokuwa wafanya biashara ikiwemo waendesha vyombo vya moto. Amesisitiza kuwa endapo mtu yeyote hatohakiki TIN namba kwa muda ulioongezwa utafutwa katika mfumo wa mamlaka hiyo na kulazimika kuomba tena.

“Tumeongeza muda kutoka mwezi wa kumi hadi kufika tarehe 30 mwezi Novemba ni kutokana na msongamano ambao umejitokeza kwa siku za mwisho mwisho. Tumeona kwamba idadi ya muda wa wiki moja hivi wiki mbili, msongamano umekuwa mkubwa sana katika vituo vya kuhakiki TIN zetu,” alisema Kayombo.

“Kwahiyo tumeona ni vyema kupunguza misongamano hiyo ili watu waweze kuhakiki TIN namba zao kwa nafasi lakini wengine wote ambao walikuwa hawajaweza wapate nafasi yakuweza kuhakiki TIN zao.”

BY:EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents