Burudani

Tuzo za TAYPA za zinduliwa rasmi, mchakato wa kupendekeza majina waanza

Tanzania Annual Young Professionals Awards (TAYPA) ni tuzo zinazofanyika kila mwaka ili kutambua utaalumu wa kipekee wa vijana na ufanisi wa utendaji kazi katika mashirika ya umma na binafsi na jitihada zao za kipekee zimeleta manufaa kwa jamii inayowazunguka na maendeleo ya kitaifa kwa ujumla na kuwa mfano kwa wengine.
Mratibu wa tuzo za TAYPA 2016, Irene Amos

Akuzungumza na waandishi Jumatano hii, Mratibu wa tuzo za TAYPA 2016, Irene Amos amewataka wadau mbalimbali kuanza kupendekeza majina yao huku akiwataka kuzingatia vigezo.

“Mchakato wa kuanza kupendekeza majina unaanza Ijumaa hii tarehe 1, kwa hiyo watu wazingatie vigezo tu. Mshiriki awe mwenye umri kuanzia 18 hadi 35, awe na mchango katika maendeleo ya nchi, awe ni mfano wa kuigwa katika jamii, awe mfanyakazi katika sekta yoyote iliyochangia na kuleta maendeleo ya kitaifa au jamii inayoizunguka. Pia mshiriki awe raia wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania,” alisema Irene.

Pia alisema tuzo hizi ni chanzo cha motisha kwa wataalamu vijana kufanya kazi kwa bidii katika kufanikisha malengo yao ya muda mfupi na muda mrefu.

Makundi 6 ya tuzo

Tuzo ya Sage
– Inatolewa kwa wale vijana ambao wanachangia katika maendeleo wengine kwa kuwashauri au kuwaelimisha watu ambao wameonyesha mafanikio.

Tuzo ya Trail Blazer
– Inatolewa kwa wale vijana ambao wamepata matokeo mazuri kwa kuonyesha uongozi wa kipekee katika mazingira magumu.

Tuzo ya Captain of Industry – Inatolewa kwa wale vijana ambao wanafanya mradi/miradi yenye mafanikio kwa kuonyesha uwezo wa uongozi wa kipekee.

Tuzo ya Pioneer
– Inatolewa kwa wale vijana ambao wanaonyesha uwezo wao kwa kubuni bidhaa au huduma kupitia technolojia ambazo zimeboreshwa na kurahisisha hali ya maisha kwa watumiaji kupitia uvumbuzi wake.

Tuzo ya Alliance – Zinatolewa kwa ajili ya vikundi vya vijana ambavyo vinashirikisha kwa pamoja kwenye miradi ya kimaendeleo.

Tuzo za Incubator
– Zinatolewa kwenye makampuni yenye mfumo rasmi wa kujenga vijana na kuwapa nguzo ya mwanga kuonyesha mipango katika kujitegemea.

Jinsi ya kupendekeza mshiriki katika tuzo za TAYPA 2016, tembelea tovuti www.taypa.co.tz kasha jaza fomu inayopatikana katika kipengele cha mapendekezo , kasha tuma. Zoezi hili la kupendekeza litaanza rasmi 1/04/2016 hadi 30/04/2016.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents