Burudani

UjasiriaHipHop: Fid Q ni dalali wa madini ya Ruby..

Fareed Kubanda aka Fid Q hategemii muziki peke yake. Pamoja na kuhusika kwenye miradi mbalimbali ya kijamii kama ‘Ujamaa Hip Ho Darasa’, Fid ni dalali wa madini.,

fid

“Nimeingia katika biashara ya madini ya Ruby ili kukuza kipato changu. Unajua huwezi kufanya muziki peke yake, lazima muda mwingine ujikite katika biashara zitakazokuletea faida na kipato kikubwa ili uweze kufanya maendeleo zaidi katika maisha,” Fid aliiambia safu ya Starehe ya gazeti la Mwananchi.

Fid amesema kwenye biashara hiyo anashirikiana na mfanyabiashara mkubwa wa madini wa Arusha. “Mimi nimeingia kati kama dalali, ni fursa kwangu na kwa kuwa nafahamiana na watu wengi ninaweza kufanya vizuri biashara hii.”

“Napata faida kubwa sana, ambayo imeniwezesha kuanza kufanya mambo kadhaa ya kimaendeleo, ambayo sitakuwa tayari kuyaweka wazi kwa sasa, lakini mambo yakiwa mazuri na kukamilika kwa mipango yangu, wananchi watajua tu.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents