Ujumbe wa Waziri Kigwangalla baada ya Shilole kupigwa na mume wake Uchebe

Baada ya picha kusambaa zikimuonyesha msanii wa muziki wa bongo Fleva Shilole akidai kupigwa na mume wake Uchebe, watu wengi walitoa maoni yao na mmoja ya watu waliotoa maoni yake ni Waziri wa Mali asili na Utalii Mh. Hamis Kigwangalla.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika hivi:-

“@officialshilole amefanya nini kinachostahili kipigo chote hiki? Hivi mwanaume ukiishampiga hivi mkeo utaweza kumuambia tena ‘nakupenda’? Na kumuita tena ‘honey’ , ‘love’, ‘lawalawa’, nk?! Unavyompiga hivi unakuwa umepeleka wapi upendo, huruma, ubinadamu na uanaume wako? Hakuna kosa linaloweza kuhalalisha kipigo kwa mkeo cha namna hii. Hakuna. Labda kama utuambie kwamba aliyetoa kipigo hiki ana aina mojawapo ya ugonjwa wa akili na amesahau kunywa dawa zake siku hiyo. Si vingine. Wanaume tuna wajibu wa kuwapenda, kuwahurumia na kuwahudumia wake zetu. Tutimize wajibu wetu huu siyo vinginevyo. Kama unaona mwanamke amekushinda zungumza kumuacha na ama kumrudisha kwao, ama kumruhusu aondoke, lakini siyo kumpiga. #BaloziWaWanawake #HK”

View this post on Instagram

@officialshilole amefanya nini kinachostahili kipigo chote hiki? Hivi mwanaume ukiishampiga hivi mkeo utaweza kumuambia tena ‘nakupenda’? Na kumuita tena ‘honey’ , ‘love’, ‘lawalawa’, nk?! Unavyompiga hivi unakuwa umepeleka wapi upendo, huruma, ubinadamu na uanaume wako? Hakuna kosa linaloweza kuhalalisha kipigo kwa mkeo cha namna hii. Hakuna. Labda kama utuambie kwamba aliyetoa kipigo hiki ana aina mojawapo ya ugonjwa wa akili na amesahau kunywa dawa zake siku hiyo. Si vingine. Wanaume tuna wajibu wa kuwapenda, kuwahurumia na kuwahudumia wake zetu. Tutimize wajibu wetu huu siyo vinginevyo. Kama unaona mwanamke amekushinda zungumza kumuacha na ama kumrudisha kwao, ama kumruhusu aondoke, lakini siyo kumpiga. #BaloziWaWanawake #HK

A post shared by Dr. Hamisi Kigwangalla (@hamisi_kigwangalla) on

Related Articles

Back to top button