Bizzare

Ukata wa Pesa: Walimu walipwa vifaranga badala ya mshahara

Wakati nchini Tanzania walimu wakiomba kuongezewa mishahara, Mji mmoja nchini Uzbekistan umekua ukiwapa waalimu wake kuku kama mshahara badala ya pesa.
Buff Bantam Hen {Gallus gallus domesticus} with nine of her ten chicks, 2-days-old. The tenth chick is under her
Mamlaka za mji wa Nukus katika jimbo linalojitawala la Karakalpakstan wamekua wakitia vifaranga wachanga kwa walimu kutokana na uhaba wa pesa nchini humo.

Kituo cha radio kinachofadhiliwa na Marekani{Radio Ozodlik} kimemnukuu mwalimu mmoja akilaani hatua hiyo kama aibu kubwa kwa mamlaka.

Mwalimu huyo aliyeghadhabishwa na hatua hiyo amesema hataki vifaranga kwa sababu anaweza kuwapata sokoni, lakini wanataka pesa zao.

Vifaranga wanaotolewa kama mshahara wana gharama ya dola mbili kila mmoja, ikiwa ni maradufu bei inayouzwa vifaranga sokoni.

Mamlaka za Uzbekistan hazikubalii uhuru wa vyombo vya habari na raia wa huko hutegemea vyombo vya habari vya kimataifa kutoa sauti yao, ila hawajitambulishi.

Uzbekistan imekumbwa na uhaba wa fedha kwa miaka sasa hali inayosababisha serikali kuchelewesha mishahara ya wafanyikazi na malipo ya uzeeni.

Mapema mwezi huu wafanyikazi wa serikali katika mji mkuu,Tashkent walilalamikia kwamba hawakuwa wamelipwa mshahara kwa miezi miwili kwa sababu benki hazikuwa na pesa.

Source:BBC

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents