Habari

Ulipitwa? Tazama hapa habari mpya kutoka vituo vya televisheni vya Tanzania (Video)

Naibu waziri ofisi ya waziri mkuu muungano na mazingira aiagiza NEMC na halmashauri ya jiji la Mwanza kubaini waliojenga mabondeni.

Zaidi ya wakazi 28 waliosahaulika kwenye ulipaji wa fidia kwenye maeneo yalichukuliwa na TPDC kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda cha mbolea waililia serikali.

Wananchi wilayani Rungwe mkoani Mbeya waiomba serikali kuwajengea daraja kufuatia daraja lilipo hivi sasa kuwa hatarishi kwa maisha yao.

Serikali ya Tanzania imekarbisha wawekezaji kwenye sekta ya umeme na viwanda baada ya kupata zaida ya gesi asilia futi za ujazo zaidi ya milioni 100 kwa siku.

Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es salaam wamekuwa na maoni tofauti juu ya maadhimisho ya sikukuu ya mapinduzi Zanzibar huku wakitoa rai kusuluhisha mgogoro uliopo Zanzibar.

Rais Dkt. Ali Mohammed Shein aongoza watanzania katika sherehe ya maadhimisho ya miaka 52 ya mapinduzi ya Zanzibar;

Wananchi mkoani Tabora waadhimisha miaka 52 ya mapinduzi ya Zanzibar kwa kufanya usafi wa mazingira mkoani humo;

Mkazi mmoja wa Iringa amefariki kwa kuangikiwa na ukuta wa nyumba na mwingine kunusurika kifo kufuatia mvua kubwa iliyonyesha mkoani humo;

Waziri wa afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto, Mhe.Ummy Mwalimu avipandisha hadhi vituo viwili vya afya vilivyopo wilayani Songea mkoani Ruvuma;

Klabu ya Simba ya jijini Dar es Salaam yamfuta kazi kocha mkuu, Dylan Kerr pamoja na benchi zima la ufundi;

Mshambuliaji Mbwana Samata asema inahitajika mipango maalum katika kuiboresha timu ya taifa ya Taifa Stars;

Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohammed Shein awahimiza wananchi kuendelea kudumisha amani visiwani humo;

Serikali yaifutia leseni kampuni ya wakala wa ajira ya Salama Investment Limited iliyoko mkoani Mwanza kwa kukiuka sheria ya ajira nchini;

Serikali yawatoa hofu wananchi wa Gongo la mboto kuhusu zoezi la bomoabomoa inayoendelea jijini Dar es Salaam;

Baadhi ya wakazi wa Shinyanga wamejikuta katika wakati mgumu baada ya mvua zinazoendelea kunyesha mkoani humo kuharibu miundombinu; https://youtu.be/46_d4zpA8sc

Halmashauri ya wilaya ya Nzega yafunga maduka 400 kwa madai ya wamiliki wa maduka hayo kukaidi kulipa kodi;

Timu ya Coastal Union ya Tanga yamtangaza kocha Ali Jangalu kuwa mrithi wa Jackson Mayanja aliyejiunga na timu ya Simba;

Kocha Louis Van Gaal ajitetea kuhusu mashabiki kuwahi kuondoka uwanjani wakati wa mchezo baina ya Manchester United na Sheffield United wiki iliyopita;

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents