Habari

Ulipitwa? Tazama hapa habari mpya kutoka vituo vya televisheni vya Tanzania (Video)

Serikali yapiga marufuku uuzaji na ubadilishaji wa fedha katika maeneo yasiyo rasmi;

Waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi, Mhe. William Lukuvi asema wilaya ya Bagamoyo inaongoza kwa uuzwaji holela wa ardhi;

Wananchi mkoani Iringa wameutaka uongozi mkoani humo kuimarisha miundombinu ili kuepuka athari zitokanazo na mvua;

Mkuu wa mkoa wa Tanga, Mwantumu Mahiza amemuagiza mkuu wa wilaya ya Tanga kusimamia malipo ya vibarua wa bandari ya Tanga ili waweze kulipwa sawa na maagizo ya serikali;

Inaelezwa kuwa pato la taifa la Tanzania laongezeka zaidi kwa asilimia 6.3 katika kipindi cha januari hadi septemba 15 kwa mwaka 2015;

Kocha wa timu ya Yanga, Hans van Pluijm amekanusha uvumi ulioenea kuwa wachezaji wa timu hiyo waligoma kupiga penati wakati wa mchezo baina ya Yanga na URA;

Waziri mkuu Kassim Majaliwa amemtembelea na kumpa pole mama Maria Nyerere kwa kufiwa na mkwewe marehemu Leticia Nyerere;

Mtoto mmoja wilayani Geita auawa kwa kuliwa na mamba alipokuwa akifua nguo pembezoni mwa ziwa Vickitoria;

Serikali mkoani Dodoma imesitisha zoezi la ubomoaji vibanda katika soko kuu la Majengo mpaka pale itakapotoa maeneo mengine kwa ajili ya kina mama lishe;

Mahakama ya Kisutu ya jijini Dar es Salaam imeitupilia mbali kesi iliyofunguliwa na mkazi wa Dar es Salaam,Elias Newala kuhusu kuzuia kwa muda uchaguzi wa mameya kwa manispaa ya Ilala na Kinondoni;

Serikali imesema itaanza kuwatoza kodi wamiliki wa nyumba za kupanga katika kuongeza pato la taifa;

Serikali yalishauri shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF kumtengenezea kumbukumbu mshindi wa tuzo ya mchezaji bora Afrika, Mbwana Ally Samatta;

Siku kadhaa baada ya kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa dunia, Lionel Messi aonekana uwanjani akifanya mazoezi kwa ajili ya mchezo baina ya Barceleona na Espanyol;

Waziri ardhi William Lukuvi aagiza manispaa ya Ilala kuvunja jengo la ghorofa 16 baada ya kubainika kuwa na kasoro nyingi.

Mtoto mmoja wa kata ya Nyambonge mkoani Geita afariki dunia baada ya kuliwa na mamba wakati akiosha vyombo katika mwambao wa ziwa Victoria.

Chama cha mpinduzi CCM chasisitiza kwamba ajenda ya kupinga ufisadi na rushwa nchini kama inavyotekelezwa na Rais Magufuli ni ya chama hicho kinyume na madai ya vyama vya upinzani.

Pato la taifa laelezwa kuendelea kukua katika kipindi cha mwezi Julai na Septemba 2015 kwa kasi ya asilimia 5.3.

Mwenyekiti wa chama cha watu wenye ulemavu wa ngozi aitaka serikali kufanya uchunguzi kuhusiana na kupotea kwa mtoto mwenye ulemavu wa ngozi.

Jeshi la polisi la Dar es salaam latoa onyo na tahadhari kwa watumishi wa benki wanao kula njama na majambazi ili kuvamia na kupora wateja wanaochukua fedha katika benki hizo.

Chama cha mapinduzi CCM, chajitokeza na kuipinga Chadema juu ya ajenda ya ufisadi na rushwa huku kikimkalia kooni Tundulisu.

Waziri wa nishati na madini Prof.Sospeter Muhongo aiagiza kampuni ya uchimbaji wa makaa yam awe ya Ngaka TANCO kukaa meza moja na Tanesco na kukubaliana gharama za kuuziana umeme kwa bei nafuu.

Chama cha walimu mkoa wa Dodoma chaiomba serikali kutatua changamoto zinazowakabili walimu wanaostaafu ikiwemo kutowarudisha makwao wanapostaafu.

Baraza la waislamu Tanzania BAKWATA, lasema kuanzia sasa shughuli zote za UMRA ama HIJJA ndogo zitakuwa zinaratibiwa na baraza hilo.

Bodi ya mikopo ya wanafunzi ya elimu ya juu hapa yaelezwa kuvuka malengo ya utoaji mikopo toka uanzishwaji wake.

Waendesha bodaboda jijini Dar es salaam wafanya maandamano kuelekea kwa mkuu wa mkoa ili kutoa kilio chao cha kunyanyaswa na askari wa usalama barabarani.

Bunge la jumuiya ya Afrika mashariki lauvalia njuga mgogoro wa Burundi huku likipokea maaombi maalum kutoka kwa wananchi wa Burundi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents