Habari

Umoja wa Mataifa juu ya mauaji Sudani Kusini

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS umelaani mauaji ya mmoja wa wafanyakazi wake nchini humo.

Charles Kiir Gone alikuwa akihudumu na misheni ya kulinda amani huko Wau, kaskazini-magharibi.

Inasemekana aliuawa wakati wa shambulio la watu wenye silaha katika nyumba ya jamaa, ambapo alikuwa akiishi.

Bw Gone alikuwa likizoni kutoka kazini wakati wa shambulio hilo ambalo limehusishwa na wizi wa mifugo, kulingana na tovuti ya habari inayomilikiwa na kibinafsi ya Eye Radio.

UNMISS imetoa pole kwa familia na imezitaka mamlaka kuchunguza mara moja tukio hilo.

Katika taarifa, mkuu wa UNMISS Nicholas Haysom alisema shambulio hilo “linaonyesha tishio halisi na linaloendelea kwa maisha ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa wanaoiunga mkono Sudan Kusini katika safari yake ya kuelekea amani”.

Mzunguko mbaya wa uvamizi wa mifugo na mashambulizi ya kulipiza kisasi umekumba Sudan Kusini, huku maelfu wakiuawa katika miaka ya hivi karibuni.

Chanzo: BBC SWAHILI
Imeandikwa na Mbanga B.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents