Habari

Upatikanaji wa dawa nchini umeimarika – Dr Kigwangalla

Serikali kupitia Wizara ya Afya ,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia, Wazee na Watoto imesema kuwa hali ya upatikanaji wa dawa nchini sasa imeimarika na kufikia asilimia 83.


Naibu Wazara ya Afya ,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia,Wazee na Watoto, Dr Hamisi Kigwangalla

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Dr. Khamis Kigwagalla alipokuwa akijibu Hoja mbalimbali za Wabunge leo Mjini Dodoma ambapo ameishukuru serikali ya awamu ya tano kwa kufanya boresho hilo.

“Moja wapo ya vipaumbele vya Serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Mheshimiwa John Pombe Magufuli, ni kuboresha upatikanaji wa dawa kwenye vituo vya kutolea huduma za Afya kwa umma nchini, katika kutekeleza azma hii serikali ya Awamu ya Tano ni kuboresha upatikanaji wa dawa kwenye vituo vya kutolea huduma ya afya kwa umma hapa nchini ” amesema Mhe. Kigwangalla.

“Katika kutekeleza azma hii serikali ya Awamu ya Tano ilichukua juhudi za makusudi kwa kuongeza bajeti ya dawa kutoka shilingi Bilioni 31 katika mwaka wa fedha 2015/2016 hadi kufikia shilingi Bilioni 251.5.Kufuatia ongezeko hilo la fedha hali ya upatikanaji wa dawa nchi imeimarika na kumbukumbuku zilizopo katika wizara ya afya, jinsia,wazee na watoto zinaonyesha kuwa hali ya ongezeko nchini imeimarika kwa kufikia asilimia 83.”

Aidha Dr Kigwangalla alisema hadi kufikia April, 2017 Jumla ya Bilioni 112 zilikwisha kutolewa na kupelekwa Bohari ya Dawa ili kuviwezesha vituo vya kutolewa huduma za Afya vya Umma kupata mahitaji yake ya Dawa,Vifaa,Vifaa tiba na Vitendanishi.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents