Michezo

USAJILI: Torres, aongeza mkataba Atletico Madrid

Mshambuliaji wa klabu ya Atletico Madrid ya nchini Hispania, Fernando Torres ameamua kuongeza mkataba wa mwaka mmoja kuendelea kuitumikia timu hiyo utakaomfanya asalie mpaka Juni mwaka 2108.

Mchezaji wa klabu ya Atletico Madrid na timu ya taifa ya Hispania, Fernando Torres

Atletico imethibitisha kumuongezea mkataba mchezaji huyo wa zamani wa majogoo wa Landani, Liverpool utakaomfanya aendelee kuitumikia klabu hiyo katika msimu ujao wa ligi kuu nchini Hispania (LA LIGA).

Mchezaji huyo wa timu ya taifa ya Hispania mwenye umri wa miaka 33, alihusishwa kuihama klabu hiyo na sasa amedhihirisha kuendelea kuitumikia Atletico Madrid ambayo ameifungia jumla ya magoli 28 tangu arejee katika viunga vya Vicente Calderon.

By Hamza fumo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents