Habari

Utafiti: Kutazama sana TV kunasababisha magonjwa haya

Utafiti mpya unaohusishwa na utazamaji wa TV uliopitiliza ufikao saa nane kwa siku unaweza kusababisha magonjwa hatari kama saratani, ugonjwa ini na Parkinson’s (kutetemeka).

couple-watching-tv-main

Watafiti kwenye taasisi ya taifa ya saratani, Michigan Marekani walibaini kuwa wale wanaotazama TV kwa saa tatu na nusu kwa siku hawapo kwenye hatari pekee ya kupata saratani au magonjwa ya moyo, bali pia kisukari, mafua na Pneumonia.

Kuangalia TV kwa saa saba kwa siku kunamwacha mtu akiwa na asilimia 47 ya hatari ya kupata magonjwa hayo juu. Wanasayansi walizingatia pia mambo mengine hatari kiafya kama vile ulaji usio na afya, uvutaji wa sigara na unywaji pombe.

Hata hivyo walibaini kuwa pale tabia hizo zilipoondolewa, hatari za kukaa na kuangalia TV zilibaki pale pale.

“Even if people were active when they weren’t watching television, they were still more likely to die from illness than natural causes if they spent a lot of time watching the box,” ulisema utafiti huo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents