Burudani

Video: Gigy money kuachia video ya wimbo ‘Tikisa Supu’, ataka watoto wakae mbali

Msanii wa muziki, Gigy Money anatarajia kuachia video yake mpya ya wimbo ‘Tikisa Supu’, ambapo amewataadharisha watoto kukaa mbali na kazi hiyo.
Gigy

Muimbaji huyo ambaye pia ni video queen, ameiambia Bongo5 Ijumaa hii kuwa ameamua kuachia wimbo ‘Tikisa Supu’ baada ya kuona tayari kuna watu wengi ameshaimba nyimbo za kutikisa sehemu za miili yao.

“Unaniuliza kucheza, nitikise nini?, maana watu wameshatikisa kiuno, mapaja, nitikise matiti?, no, hawataki. Nitikise Supu, wanataka. Kwa hiyo kwa lugha za kwenye runinga nikisema nitikise makalio haitaleta picha nzuri, na nyimbo naihisi itapendwa sana,” alisema Gigy.

Video ya wimbo ‘Tikisa Supu’ utatoka katikati ya mwezi huu baada ya kukamilika kwa matayarisho ya mwisho.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents