Burudani

Video: Going Bongo kuwa filamu ya kwanza Afrika Mashariki kukubalika kuuzwa kupitia iTunes

Filamu ya Going Bongo inatarajiwa kuwa filamu ya kwanza Afrika Mashariki kukubalikwa kuuzwa kupitia mtandao wa iTunes. Filamu hiyo itaanza kuuzwa kupitia iTunes July 10 mwaka huu.

https://www.youtube.com/watch?v=m4KwGVe4tj8

Going Bongo ni filamu ya kwanza kufanyika nchini Tanzania kuhusu daktari wa Marekani (nafasi iliyochezwa na mtanzania Ernest Napoleon aka MC Napo) ambaye ana hamu ya kumfurahisha bosi wake katika kazi yake kwenye hospitali ya Beverly Hills jijini Los Angeles.

promo7jpg
Ernest Napoleon

Itazame trailer ya filamu hiyo hapa:

https://www.youtube.com/watch?v=So0QIUM6kOM

Baada ya kuhudhuria hafla iliyoanzishwa na bosi wake, anajikuta anajitolea kimakosa kwenda kufanya kazi kwenye hospitali ya Tanzania yenye hali ngumu kwa mwezi mzima.

promo4

Filamu hiyo itazinduliwa Dar, August mwaka huu.

promo6

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents