Burudani

Video: Kama Media zitakataa kutulipa tunaweza kugoma – Babu Tale

Meneja wa Diamond Platnumz, Babu Tale amesema haamini katika kugoma kama njia ya kutafuta haki bali njia sahihi ni kukaa meza moja ya kutafuta suluhisho.

Akizungumzia suala la wasanii kulipwa mirabaha na vyombo vya habari pindi vinapocheza kazi zao, hoja iliyoibuliwa katika mkutano kati ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe na wasanii wa muziki. Babu Tale amesema si sawa kwa wasanii kugoma kama ilivyopendekezwa na baadhi ya wadau bali kutafuta suluhisho kwa mazungumzo.

“Sijamuona mgomaji, off course tuna tatizo la kupigania wasanii wapate haki yao lakini haki haiendi kwa kugoma, haki inaenda kwa kukubaliana jambo moja kwenda jambo jingine, lakini tukisema wagome, tunaweza tukagoma, halafu!!, nani anapoteza, wao au sisi?, lakini tukae pamoja sisi na watu wa media house tuwaambie hiki kinachopangwa ni sawa au si sawa,” Babu Tale ameiambia Bongo5 na kuongeza.

“Lakini hata Waziri amezungumza gharama ambayo inatozwa ni kubwa, hata wakitaka watulipe ni kiasi kikubwa sana (hawataweza), basi kingepunguza ila kinapoenda mara kwa mara kingekuwa kikubwa na kingetutosha,” amesisitiza Babu Tale.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents