Habari

Video: Mizengo Pinda apewa shavu kwenye The Colbert Report ya Comedy Central.. lakini si kama unavyodhani

Kutajwa kwenye show kubwa inayotazamwa kwenye channel ya TV inayoangaliwa mno nchini Marekani, Comedy Central si kitu cha kuchukulia poa hasa kama aliyetajwa ni Mtanzania.

Mtangazaji wa kipindi cha The Colbert Report, Stephen Colbert jana amempa shavu waziri mkuu wa Tanzania, Mizengo Pinda wakati akikikosoa kitabu cha mke wa rais wa zamani wa Marekani, Bill Clinton, Hillary Rodham Clinton ‘Hard Choices’.

Colbert anadai kuwa pamoja na kitabu hicho kuwa na kurasa 656, kimejaa utajaji hovyo wa majina huku sehemu moja akisema ‘Mimi na Waziri Mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda tunapanda miti kwenye chama cha wanawake huko Mlandizi’.

Hata hivyo mtangazaji huyo aliwasurprise zaidi watazamaji aliposema: “There is no way on earth one woman can be in so many places at once’ na muda huo Clinton akaingia studio hapo na kusababisha shangwe zito.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents