Habari

Video: Moto mkubwa wateketeza jengo la makazi London

Moto mkubwa umeteketeza jengo moja la makazi katika barabara ya Latimer magharibi mwa London, na wanaoshuhudia wanadai kuwa watu wamekwama manyumbani mwao.
https://youtu.be/lVI2D_FFMms
Moto huo katika jengo la Grenfell Tower ulianza mwendo wa saa 01:16, saa za Uingereza na karibu wazimamoto 200 wanapambana nao.

Polisi wanasema kuwa watu kadhaa wanadaiwa kukimbizwa hospitali.

Mwandishi wa BBC anasena jengo hilo lote limeshika moto na kuna hofu kuwa huenda likaporomoka.

Idara ya wazima moto jijini London imetuma malori 40 ya kuzima moto huo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents