Habari

Video: Wote tunapenda Lissu apone – Waziri Ummy

Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maaendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, imesema serikali iko pamoja na Watanzania kwasababu watu wote wanapenda Mhe. Tundu Lissu apone na aendelee na shughuli zake za kila siku.

Akizungumza na Waandishi wa habari mjini Tanga jana, Waziri wa Afya, Maaendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu alisema serikali inasubiri maombi rasmi kutoka kwa mke wa Lissu (Alice)pamoja na familia yake na barua kutoka kwa madaktari.

“Dada angu Alice ambaye ni mke wa Lissu namtaja kwa jina nasubiri rasmi kupata maombi yako , familia ya Lissu tuko tayari kupata maombi yenu kama serikali tuko pamoja na nyie kama Watanzania kwasababu wote tunampenda Lissu apone aendelee na shughuli zake za kila siku,” alisema Waziri Ummy.

Lissu alijeruhiwa kwa kupigwa risasi Septemba 7 na watu wasiojulikana katika eneo la ‘area D’ mjini Dodoma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents