FahamuHabari

Vikosi vya Marekani nchini Iraq vyashambuliwa na ndege zisizo na rubani

Roketi na ndege zisizo na rubani zilipiga kambi za kijeshi za Iraq zinazohifadhi wanajeshi wa Marekani siku ya Alhamisi, kulingana na shirika la habari la Reuters likinukuu vyanzo vya usalama ambavyo havikutajwa.

Milipuko mingi ilisikika ndani ya kambi ya jeshi la anga ya Ain al-Asad na jeshi la Iraq limefunga eneo hilo na kuanza msako, Reuters imeripoti. Haijulikani ikiwa kulikuwa na majeruhi kutokana na mashambulizi haya.

Haya yanajiri baada ya makundi yenye silaha ya Iraq yanayoungana na Iran kutishia wiki iliyopita kulenga Marekani kutokana na uungaji mkono wake kwa Israel dhidi ya Hamas.

Mapema siku ya Alhamisi, Pentagon ilisema kuwa majeshi ya Marekani nchini Iraq na Syria yamekuwa yakikabiliwa na mashambulizi mengi ya ndege zisizo na rubani tangu Jumanne.

Walisababisha majeraha madogo, ingawa mwanakandarasi raia alikufa baada ya kupata “mshtuko wa moyo” wakati akijikinga na tishio linalowezekana.

Msemaji wa Pentagon Brigedia Jenerali Pat Ryder alisema “wameona wanamgambo wanaoungwa mkono na Iran wakifanya mambo ya aina hii”, lakini akaongeza kuwa bado wanatathmini mashambulizi hayo na hawana maelezo zaidi.

Pentagon pia ilisema huko Yemen, meli ya kivita ya Marekani ilidungua makombora na ndege zisizo na rubani zilizorushwa na vikosi vya Houthi, vilivyolenga “uwezekano wa shabaha za Israeli”.

Ryder alisema watachukua hatua “kulinda na kutetea washirika wetu na maslahi yetu” na lengo lao lilikuwa “kuepuka upanuzi wowote wa kikanda wa mzozo wa Israeli na Hamas”.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents