Vitendo vya wanaume kuomba namba za simu za wanawake barabarani kupigwa marufuku

Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron yupo tayari kupitisha sheria inayozuia wanaume kuomba namba za simu za wanawake hadharani ili kupunguza vitendo vya udhalilishaji.

Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron wa pili kutoka kushoto akiwa na wanaharakati Malala na Marlene Schiappaā€¸ kutoka kulia.

Rais Macron (39) mwaka jana wakati wa kampeni zake aliahidi kufuta baadhi ya sheria ambazo zinawakandamiza wanawake nchini Ufaransa ikiwemo ile inayokataza wanawake wa dini ya Kiislamu kuvaa hijab na niqab na aina nyingine ya vitendo vya udhalilishaji kwa wanawake.

Katibu wa Wizara ya Usawa na Jinsia nchini Ufaransa na Mshauri wa Ofisi ya Rais, Bi Marlene Schiappa amesema muswada wa sheria hiyo utapitishwa haraka na kusainiwa na Rais kama alivyoahidi kwenye kampeni zake kwani wanawake nchini humo wamekuwa wahanga wakubwa wa vitendo vya udhalilishaji.

Taarifa iliyotolewa na Tovuti ya Wizara hiyo imeeleza kuwa Kamati ya Wabunge wanne tayari imekaa kujadili muswada huo kwa kina kabla ya kupeleka kwa Rais Macron.

Tayari serikali katika kupiga vita vitendo hivyo vya udhalilishaji imetoa namba za simu za kupiga bure kwa Wanawake watakaofanyiwa vitendo vya udhalilisha ikiwemo kuomba namba za simu, kuwapigia miluzi, ubakaji, kutukanwa au vitendo vyovyote vinavyoashiria udhalilishaji wa kijinsia.

Hata hivyo, wanaume wengi nchini humo wamepinga sheria hiyo wakisema kuwa kufanya hivyo ni kuharibu baadhi ya tamaduni zilizozoeleka maarufu kama macho (Macho Culture).

 

Related Articles

Back to top button