Habari

Vyama vitatu vya siasa vyafutiwa usajili

Msajili wa vyama vya siasa nchini amevifutia usajili wa kudumu vyama vitatu vya siasa kikiwemo chama cha haki na ustawi (CHAUSTA), chama cha African Progressive Party of Tanzania (APPT), na chama cha Jahazi Asilia baada ya zoezi la uhakiki wa vyama lililofanyika Juni 26 mpaka tarehe 26 Julai.

jaji-francis-mutungi-620x420

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, msajili wa vyama vya siasa nchini, Jaji Francis Mutungi, amesema kuwa amevifutia vyama hivyo kutokana na zoezi la uhakiki wa vyama ya siasa.

“Nimefuta usajili vyama vitatu vya siasa vifuatavyo kuanzia leo hii tarehe 9 Novemba 2016. Chama cha kwanza kinaitwa CHAUSTA,kilichopata usajili wa kudumu Novemba 2001 ambacho kilikuwa kinaongozwa na Bwana James Mapalala kama mwenyekiti wa taifa. Chama cha pili APPT Maendeleo, kilichopata usajili tarehe 4 Marchi 2003 ambacho kilikuwa kinaongozwa Bwana Peter Kuga Mziray kama rais mtendaji taifa. Chama cha tatu ni Jahazi Asilia kilichopata usajili tarehe 17 Novemba 2014 kilichokuwa kinaongozwa na Bwana Kassim Bakari Ally kama mwenyekiti wa taifa,”amesema Jaji Mutungi.

“Mchakato wa kufuta usajili wa vyama hivi unatokana na zoezi la uhakiki utekelezaji wa masharti ya usajili na matakwa na sheria ya vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu uliofanyika kuanzia tarehe 26 Juni mpaka tarehe 26 Julai 2016 Katika zoezi hilo la uhakiki lilibaini kuwa vyama vya siasa hivyo vimepoteza sifa za usajili wa kudumu kwa kukiuka masharti ya vyama vya siasa,”ameongeza.

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents