Habari

Wafanyakazi wanalia, wafanyabiashara, watu wote wanalia inawezekanaje?- Mbunge ahoji (+video)

Mbunge wa Kuteuliwa(CCM), Abdallah Bulembo amesema kuwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina hawatendei haki Watanzania hasa sekta ya uvuvi kwa Operation ya uvuvi haramu aliyomtaka aisimamishe kwa kile alichodai inaumiza wavuvi.

Bulembo ameyasema hayo, wakati akichangia Bajeti ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi ya mwaka 2018/019 ambapo amesema haiwezekani Wafanyakazi wanalia, wafanyabiashara, watu wote wanalia inawezekanaje?

Aidha Bulembo aliongeza kuwa Kama Waziri hawasikilizi watu wa seta yake Uwaziri wake ni nini? alihoji kwa uchungu.

“Kuna wavugaji wapo hapo nje wanalalamika ngo’mbe wao wameuzwa, hii haipo ndani ya Ilani ya CCM kwamba Waziri utakuwa baada ya kumsaidia Rais unamsababishia matatizo, Msimchanganye Rais na Rais hawezi kushangilia wananchi wanateswa, hawezi kushangilia wananchi wake wanaumizwa, Rais amepigiwa kura anatakiwa kurudi kuomba kura kule kwanini mnamchanganya Rais na matatizo ya mtu mmoja ambaye ni Waziri?,” alihoji.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents