Burudani

Wageni waalikwa kwenye harusi ya Kanye na Kim kupewa zawadi zenye thamani ya tshs milioni 200!!

Kwa kawaida harusi za kibongo, picha huaanza kwa mchango wa harusi na siku ya sherehe ni lazima uende na zawadi ya kuwatuza maharusi. Lakini hiyo sio kwenye harusi ya Kanye West na Kim Kardashian inayotarajiwa kufanyika mwezi ujao.

Kim and Kanye

Wageni waalikwa kwenye harusi hiyo ndo watakaopata zawadi. Mpaka sasa mastaa kibao wanadaiwa kususa kuhudhuria harusi hiyo lakini sasa inabidi wafikirie kubadili mawazo yao kwani watakosa vinono. Wawili hao wanadaiwa kutumia mamilioni ya dola kwaajili ya kuwafurahisha tu wageni waalikwa ambapo kila mmoja katika wageni 200 atapokea zawadi zenye thamani $125,000 kwenye sherehe hiyo.

Mtandao wa Grazia UK umedai kuwa wapenzi hao wametumia takriban dola milioni 25 kununua zawadi za wageni peke yake. Kwenye vibegi hivyo vya zawadi kutakuwa chupa za champagne ya Bollinger ambapo moja inauzwa $500, bidhaa za Creme de la Mer zinazouzwa $200, urembo wa kutengeneza kwa mikono wenye majina ya Kim na Kanye, na zawadi zingine kibao. Pia kadi za mwaliko zinadaiwa $1,000.

Mastaa kibao wakiwemo Beyonce, Robin Thicke, Jonah Hill, Karl Lagerfeld, Oprah Winfrey na Anna Wintour wanadaiwa kugomea mwaliko.

Soma zaidi hapa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents