FahamuHabari

Wakenya walalamika kupanda kwa bei za mafuta

Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Petroli nchini Kenya (Epra) imetangaza kupanda kwa bei ya mafuta kwa Sh9 katika ukaguzi wake wa kila mwezi.

Kwa muda wa mwezi mmoja ujao, lita moja ya petroli kubwa jijini Nairobi itagharimu Sh159.12, dizeli Sh140 na mafuta taa Sh127.94, hivyo kuashiria kupanda zaidi kwa bei ya mafuta.

Aitangaza kupanda kwa bei hiyo siku ya Jumanne, Epra ilisema katika taarifa yake kwamba serikali itatumia Hazina ya Maendeleo ya Petroli (PDL) kuwaepusha watumiaji kutoka kwa bei hizo za juu.

Huku madereva wa Nairobi wakilipa Sh159.12 kwa lita moja ya petroli, bei halisi ni Sh184.68, kumaanisha kuwa serikali italipa Sh25.76 kama ruzuku .

Serikali imetangza kwamba ruzuku ya dizeli ni Sh48.19 kwa lita huku ile ya mafuta ya taa ikiwa ni Sh42.43 kwa lita.

Epra imesema bei hizo zinajumuisha kodi na zimerekebishwa kuingiliana na mfumuko wa bei.

Na punde tu baada ya tangazo hilo kufanywa Wakenya waliingia katika mitandao ya kijamii na kutoa ghadhabu zao.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents