Bongo5 ExclusivesFahamuHabariSiasa

Wamasai waandamana Dar, Kenya msitugombanishe na Serikali yetu

Wamasai waandamana mpaka katika ubalozi wa kenya nchini Tanzania kuiomba Serikali ya Kenya kuacha kuingilia na kutoa upotoshaji katika zoezi la kuwahamisha wamasai Loliondo na Ngorongoro.

Wamasai hao wamefanya maandamano ya amani hadi ubalozi wa Kenya nchini Tanzania uliopo Oysterbay jijini Dar Es Salaam leo juni 17 mwaka 2022 kuiomba Serikali ya Kenya kuacha kuingilia zoezi linaloendelea Loliondo la kuwahamisha wamasai na kuwapelekea katika ameneo yaliyotengwa na Serikali.

Wameeleza kuwa Upotoshaji huo umelenga kuichonganisha jamii ya Kimasai n aserikali ya Tanzania pamoja na kuzorotesha zoezi zima la jitihada za Serikali pamoja na makubaliano yaliyofanyika katika pande zote mbili.

Akiongea na wana habari mtu mmoja ambaye alijitambulisha kama msemaji wao LOISHIYE LASHILUNYE amesoma barua ya wazi na kueleza yafuatayo.

“HATUA HII INAKUJA BAADA YA ZOEZI LA KUWEKA ALAMA ZA MIPAKA KATIKA ENEO LA LOLIONDO PAMOJA NA UHAMAJI WA WANANCHI WA NGORONGORO AMBAPO LICHA YA SERIKALI KUTANABAISHA UWEPO WA MAKAZI MAPYA KATIKA ENEO LA HANDENI, KUMETOKEA UPOTOSHAJI NA UCHOCHEZI UNAOLENGA KUKWAMISHA ZOEZI HILO.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents