Habari

Wananchi wasio na vyoo Tabora kukamatwa

Mkuu wa wilaya ya Igunga mkoani Tabora, John Mwaipopo amewaagiza watendaji wa vijiji na kata wilayani hapo kuwasaka na kuwakamata wananchi wote wasiokuwa na vyoo katika nyumba zao.

Kauli hiyo aliitoa Jumapili hii wilayani humo, wakati akizungumza na wananchi baada ya uzinduzi wa Kituo cha Afya Choma pamoja na jengo la upasuaji, ambapo alisema wapo baadhi ya wananchi wamekuwa wakijisaidia kwa kuchimba mashimo mafupi, jambo ambalo ni hatari kwa afya zao.

“Kuanzia sasa kila mtendaji wa kijiji na kata anatakiwa kuwakamata watu wasiokuwa na vyoo na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria na mtendaji atakayeshindwa kutekeleza agizo hili hatua kali zitachuliwa dhidi yake,” alisema Mwaipopo.

Siku za hivi karibuni Mkuu wa wilaya ya Chunya, Rehema Madusa alitoa mwezi mmoja kwa kila Kaya isiyo na choo kutozwa faini wilayani humo ili kuepuka magonjwa ya mlipuko.

BY: Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents