Burudani

Wasanii wachanga kunufaika pia na uchezwaji wa nyimbo zao

Baada ya Chama cha Haki Miliki Tanzania (COSOTA) pamoja na kampuni ya kusimania haki miliki za wasanii, Copyrights Management East Africa Limited (CMEA) kutangaza neema kwa wasanii kuanza kunufaika kwa kulipwa mirahaba itokanayo na kazi zao kuchezwa kwenye redio na TV, wasanii wachanga wameanza kuwa na hofu na mfumo huo.

Muziki Pesamuziki pesa

Akizungumza na 255 ya XXL kupitia Clouds FM, Afisa Mtendaji Mkuu COSOTA, Doreen Anthony alisema kila kazi ya msanii itakayosikika itatakiwa kulipiwa.

“Kwetu sisi tunaona kwamba hii ni biashara, muziki ni biashara na redio na TV ni biashara,” alisema. “Ili wote tuweze kufaidika, msanii, TV na redio pamoja na serikali ifaidike, kwanini mtu aseme basi nisipige wimbo wa mtu ambaye anachipukia kwaajili tu ya kumkomoa ili ulisilipe? Piga mlipe achukue chake na wewe uchukue chako maisha yaendelee.” alisisitiza.

Kwa upande wa mkurugenzi mkuu wa CMEA, Paul Matthysse aka P-Funk alisema kila msanii anatakiwa kufanya kazi kwa bidii ili anufaike na kazi yake.

“Kitu kimoja unajua mfumo wetu wa Tanzania hakuna demo artist na hakuna artist mkubwa, msanii mdogo ambaye alifanya demo anaweza naye kupata airtime, nje ni ngumu hivyo,” alisema.

“Ndio maana talent inakuwa kwenye level ya hali ya juu, ukiwa bora ndio utapata nafasi zaidi ya kutoka na kusikika. Usiwalaumu media, tunachohitaji ni muziki uwe wa maana. Muziki mzuri wa kuvutia mashabiki na wasikilizaji na upigwe. Waimbaji wazuri ambao wapo kwenye hali ya juu ili tuweze kupandisha level ya muziki wetu. Kwa hiyo kaza buti, fanya kazi na wewe ufike level inayohitajika, hakuna ubaguzi wala nini kazi ikiwa nzuri ni nzuri.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents