Burudani

Wasanii wakugani wajengewa uwezo jijini Dar

Wasanii wa ushahiri na wengine chipukizi wamejengewa uwezo wa kuimba na kupata soko la kazi zao.

Mwanadada Aichieli Temu akiimba kwenye onesho hilo la muziki ambapo alizikonga nyoyo za mashabiki waliojitokeza siku hiyo

Hiyo imetokana na hatua iliyofanywa na kampuni ya Las Consultancy ambapo iliandaa oneshao lililowakutanisha wagani mashahiri na wasanii chipukizi pamoja na wadau wa muziki pamoja huku dhima ya siku hiyo ikiitwa Alternative Night.

Kwa kuwa washahiri wa kugani wengi wao wanauelewa mkubwa katika uimbaji, hivyo siku hiyo walipata nafasi ya kufanya yote hayo.

Wasanii wa muziki wa kugani Muki Bitungwa maarufu kama Mukimala (kushoto) akiimba sambamba na msanii mwenzake Salma Munde maarufu kama Sista dada kwenye onesho liitwalo Alternative night lilioandaliwa na kampuni ya las Consultancy(Picha na Evance Ng’ingo)

Ilikuwa ni katika Mgahawa wa Watering hole uliopo Masaki ambapo wasanii tisa wakimo watatu wa kugani na wengine sita wa kawaida walipata wasaha wa kugani huku wale wa kuimba wakiimba nyimbo zao mbilimbili.

Ilikuwa ni burudani safi chini ya udhamini wa kinywaji cha Hennessy huku ikipendezeshwa na mpangilio mzuri wa viti na jukwaa lililovutia kwa wadau wa muziki kuangalia onesho hilo.

Kwa kila msanii alieimba alikuwa akienda mbele ya umati huo na kisha kusimama na kuanza kugani ujumbe wake.

Walianza wasanii wa kugani ambapo msanii mwanadada Pepita Sam alianza kwa kutoa ujumbe unaowataka watu wasiziguse nywele zake.

Tukio hilo lilifuatiwa na wasani wengine kadhaa wa kuimba kama vile akina Sabi John,Teekila- Davies, Rhoda, Salma Munde,Raphael Mukimala, Bitungwa Gammaril Mtunga, Frankie Maston, Ben Mlowezi na Chi- Aichieli Temu.

Mhusika kutokea Las Consultant, Asnath Ndosi alisema kuwa kampuni hiyo imekuwa na utaratibu kama huo wa kuandaa maonesho hayo na kwa mwaka huu limefanyika mara nne.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents