Burudani

Wasiwasi wa Dogo Janja kwenye mitandao ya kijamii

Dogo Janja amefunguka na kusema kuwa katika matumizi ya mitandao ya kijamii anaogopa sana watu wanapo hariri (edit) picha na kuongeza au kupunguza kitu kwenye sura ya mtu.

Rapa huyo ambaye kwa sasa anatamba na ngoma ‘Ukivaaje Unapendeza’ amefunguka kwa kusema kwamba suala la matusi mitandaoni halimuongopeshi kutokana na mazingira aliyokulia lakini.

“Suala la kutukanwa nimezoea sana, kwani sijaanza kutukanwa jana au leo kwa sababu mazingira niliyotokea mimi baba anaweza akamtukana mama mbele ya watoto. Ila linapokuja suala la mtu kukuwekea ‘shape’ kwenye mwili wako au kukupaka make up na kukugeuza kama mwanamke huwa naogopa sana pia zinaniumiza” alifunguka

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents