Habari

Watoto nane wakutwa wamekufa kwenye gari Nigeria

Polisi nchini Nigeria wanasema wanachunguza kifo cha watoto wanane waliokuwa wamekwama ndani ya gari katika mji mkuu wa kibiashara wa Lagos.

Watoto hao, wote wavulana – wenye umri wa kati ya minne na sita walipatikana wamekufa mwishoni mwa juma.

Bado haijabainika jinsi walivyofungiwa kwenye gari lililotelekezwa. Katika taarifa, polisi katika jimbo la Lagos wanasema miili ya watoto hao imepatikana na kuhifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti kwa ajili ya uchunguzi ili kubaini sababu halisi ya kifo chao.

Taarifa hiyo inaongeza kuwa kamishna wa polisi wa jimbo hilo, Hakeem Odumosu, ameagiza ‘’uchunguzi wa kina na wa haraka ufanyike.’’

Wazazi wa watoto hao wanasemekana kuwa raia wa Niger wanaoishi Lagos. Mwenyekiti wa Wanigeria mjini Lagos, Saidu Abdullahi, aliiambia BBC kuwa watoto hao wanane wanatoka katika familia mbili.

Ametoa wito kwa mamlaka hiyo kufanya uchunguzi wa kina kuhusu mazingira ya vifo vyao.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents