HabariUncategorized

Aliyempa Sabaya milioni 90 alindwa na sheria, ombi la kina sabaya latupiliwa mbali

Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha imetupilia mbali ombi la Mawakili wa Sabaya la kutaka mahakama imkamate Shahidi wa 10 wa Jamhuri, ndg. Evarist Mrosso kwa madai kuwa alikiri mahakamani kuwa alitoa rushwa ya Milioni 90.

Sabaya akimshika bega Wakili Fidolion Bwemelo

Akisoma uamuzi mdogo leo Disemba 6, Hakimu Dk. Patricia Kisinda, amesema kuwa kifungu cha sheria ya makosa ya jinai kifungu cha 17, kilichoainishwa katika pingamizi hilo hakijñakidhi matakwa ya kuifanya mahakama itoe amri shahidi akamatwe.

Aidha, Dk. Patricia ameongezea kuwa kupitia sheria ya ushahidi ya makosa ya rushwa kifungu cha 52 kifungu kidogo cha kwanza kinamlinda shahidi na kwamba mahakama itaendelea na kumsikiliza shahidi anayefuata.

Kesi hiyo imeahirishwa mpaka kesho, ambapo upande wa Jamhuri itamleta shahidi wa 11 kuendelea kutoa ushahidi wake.

Mahakama hiyo imelazimika kutoa uamuzi huo mdogo siku ya leo baada ya Wakili wa Utetezi Fidolion Bwemelo kuiomba mahakama kumkamata Shahidi Evarist Mrosso baada ya kukiri kwamba alimpatia Lengai Ole Sabaya rushwa ya milioni 90 kwa kulazimishwa.

Sabaya na wenzake sita wanakabiliwa na kesi ya Uhujumu uchumi na. 27/2021 kwa kuchukua kiasi cha shilingi Milioni 90 kwa mfanyabiashara Evarist Mrosso Januari 22, kwa kumtishia asipofanya hivyo watampoteza au kumfungualia kesi ya kuhujumu uchumi.

Baadhi ya watuhumiwa kati ya watuhumiwa saba katika kesi ya Uhujumu uchumi.

BY : Fatuma Muna

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents