Watu saba wafariki baada ya ndege ya jeshi kupata ajali karibu na uwanja wa ndege wa Abuja (+ Video)

Watu saba wamefariki baada ya ndege ya jeshi la Nigeria kuanguka muda mfupi baada ya kupaa kutoka uwanja wa ndege, katika mji mkuu wa Abuja, asubuhi ya Jumapili, kwa mujibu wa maafisa.

Ndege hiyo ya jeshi la anga la Nigeria iliripoti kukumbwa na hitilafu katika injini yake, msemaji wa Air Vice Marshal Ibikunle Daramola, aliandika katika Twitter yake.

Aliongeza kuwa ndege hiyo ilikuwa njiani kuelekea Minna, kaskazini mwa jimbo la Niger.

Mkuu wa wafanyakazi wa shirika la ndege hiyo ameagiza uchunguzi kufanywa mara moja.

Katika msururu wa ujumbe wa Twitter, vikosi vya angani vimetoa wito kwa watu “kuwa watulivu na kusubiri matokeo ya uchunguzi”.

Ruka Twitter ujumbe, 1

Mwisho wa Twitter ujumbe, 1

1px transparent line
Ruka Twitter ujumbe, 2

Mwisho wa Twitter ujumbe, 2

1px transparent line

Msemaji wa jeshi la anga la Nigeria amesema abiria wote wamefariki.

Walioshuhudia ajali hiyo waliripoti kuona ndege ikizunguka katika eneo ilipotokea ajali kabla ya kuanguka na kushika moto karibu na barabara ya ndege ya uwanja huo. Wanasema walisikia mlio mkubwa kabla ya ndege hiyo kulipuka na kushika moto.

Mashuhuda mwingine ameiambia shirika la habari la Reuters kwamba harufu ya ndege iliyochomeka na kemikali ilisheheni sehemu ilipotokea ajali hiyo, nje kidogo ya au la uwanja wa ndege.

Bofya hapa kutazama.

https://www.instagram.com/tv/CLlbZJWh1n0/

Related Articles

Back to top button
Close