Habari

Watu wanaotafuta kazi kusafiri bure

Watu wanaotafuta kazi na wanaorudi kutoka makazini nchini Scotland watasafiri bure kwa njia ya reli.

Kampuni ya reli nchini humo ya ScotRail Alliance imesema kuwa watu wanoatafuta ajira watapata safari mbili za bure kila mwezi za kusafiri kwenda maeneo mbalimbali kutafuta kazi au kufanya usaili.

Hata hivyo Kampuni hiyo pia imetoa safari za bure kwa wale wanaopata ajira kwa mwezi wa kwanza kwa kutolipia nauli wakati wa kurudi wakitokea kazini .

Mkurugenzi wa Shirika hilo, Alex Hynes amesema msaada huo utaimarisha uchumi wa taifa hilo kwani gharama za nauli za watu wanaotafuta kazi zitafanya mambo mengine kwenye maisha yao ya kila siku.

“Kampuni yetu imejenga reli nzuri zaidi kuwahi kutokea hapa Scotland na moja ya lengo letu kubwa lilikuwa ni kuwasaidia watu katika usafiri na tumejitolea kuwasaidia watu wote wanaotafuta kazi hii itasaidia uchumi wetu kukua maradufu,”amesema Bwana Hynes kwenye mtandao wa ScotRail wa kampuni.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents