Habari

Mtatiro apewa ujumbe huu mzito na Tundu Lissu aufikishe kwa Watanzania

Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi, (CUF) Julius Mtatiro ambaye yupo nchini Kenya amesema kuwa leo Oktoba 8, 2017 amepata bahati ya kuonana na Mbunge wa Singida Mashariki, Mhe. Tundu Lissu na kupewa ujumbe aufikishe kwa watanzania wanaomuombea kila siku apone haraka.

Julius Mtatiro

Mtatiro amesema kuwa baada ya kukutana na Tundu Lissu leo (Jumapili) ameongea nae na kupewa ujumbe aufikishe kwa Watanzania.

Mtatiro nenda kawaambie kuwa nitarudi nikiwa mzima na tutaendelea na mapambano maradufu zaidi, faraja muhimu nayohitaji kutoka kwa Watanzania hivi sasa ni kuendeleza mapambano ya kudai haki na kupambana na udikteta, tusikubali nchi yetu iharibiwe na kikundi cha watu wanaoogopa kukosolewa.“ameandika Mtatiro ujumbe aliopewa na Tundu Lissu na kuuweka kwenye ukurasa wake wa Facebook.

Kwa upande mwingine Mtatiro amesema kuwa risasi zilizompata Mhe. Lissu zimemjengea uimara maradufu na kudai kuwa amejifunza mengi juu ya tukio hilo.

Risasi zote zilizopenya kwenye mwili wa Lissu zimemtengenezea uimara maradufu, mara sabini, mara mia moja. Waliodhani kuwa kumuua Lissu ndiyo kuua harakati za Watanzania kudai taifa la haki na linalofuata misingi ya sheria na katiba bora, wanajidanganya…Mimi binafsi kama Mtatiro, kumuona Lissu kumenijenga zaidi, kumenifundisha kuwa ukipigwa risasi hata 100 kwa sababu u mkosoaji wa watawala yapo mambo mawili yatatokea, aidha utapona kama Lissu au utakufa kama ilivyowatokea wapigania haki wengi.”ameandika Mtatiro kwenye ukurasa wake wa Facebook.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents