Habari

Wawekezaji watakiwa kuchangamkia fursa

Wawekezaji wametakiwa kuchangamkia fursa mbalimbali zinazopatikana katika Mkoa wa Manyara badala ya kukimbilia katika maeneo ambayo yamezoeleka na wadau wengi wa maendeleo.

Rai hiyo imetolewa leo Mjini Babati na Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara alipokuta na ujumbe kutoka Bodi ya Filamu Tanzania ukiongozwa na Katibu Mtendaji wa Bodi hiyo Bibi. Joyce Fissoo.

Kaimu Katibu Tawala huyo ameema kuwa Mkoa wa Manyara unazo fursa nyingi za uwekezaji hivyo ni vyema sasa wawekezaji wakatumia fursa hizo na kuja kuwekeza katika Nyanja tofautitofauti za uwekezaji ikiwemo kilimo, viwanda na ufugaji.

“ Mkoa wetu wa Manyara unazo fursa nyingi ambazo kama wawekezaji wakijitokeza watanufaika nazo, hivyo ni wito wangu kwao kuwa waje mkoani Manyara watumie fursa hizo, tunayo maeneo yakutosha kwa shughuli za uwekezaji”, alisema Kaimu Katibu Tawala huyo.

Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini Tanzania (KBF), Bibi. Joyce Fissoo amesema kuwa Mkoa wa Manyara ni miongoni mwa maeneo ambayo yamekuwa na mchango mkubwa katika tasnia ya Filamu nchini hasa zinazohusisha wageni kutoka nje ya nchi.

Aliongeza kuwa kitu kikubwa kinachoubeba mkoa huo ni mandhara na jiografia ya ambayo imekuwa kivutio kikubwa katika uwekezaji hasa katika eneo la utalii na filamu hapa nchini.

“ Ni jambo muhimu Mkoa wa Manyara mkajivunia kuwa na mandhari inayovutia wawekezaji, katika tasnia ya filamu wageni wengi kutoka nchi mbalimbali wamekuwa wanakuja na kuhitaji kutumia mandhari ya Wilaya ya Mbuli katika uandaaji wa filamu zao hiyo ni moja ya fursa muhimu ambayo pia itatumika kuutangaza zaidi mkoa wenu”, alisema Bibi. Fissoo.

Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania yupo mkoani Manyara kwa ziara ya kikazi kwa ajili ya kuwajengea uwezo wajumbe wa Bodi za Filamu za Mikoa na Wilaya kuhusu majukumu ya Bodi hizo na zinazoongozwa na Makatibu Tawala wa Mikoa na Wilaya.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents