Habari

Waziri Mkuu Majaliwa alivyochangisha mil 18.9 kumsaidia Mariam, Rais Magufuli apiga simu na kuchangiz mil 10 (+ Video)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameendesha harambee ya papo kwa papo na kuchangisha Sh milioni 18.9 ambapo kati ya hizo, Sh milioni 10 zimetolewa na Rais Dk. John Magufuli.

“Mheshimiwa Rais anafuatilia tukio hili na amesema anamchangia Miriam Sh milioni 10 ili ziweze kumsaidia katika mtaji wa biashara na umaliziaji wa ujenzi wa vyumba vya kupangisha”

Fedha hiyo ilichangishwa kwa ajili ya Miriam Msagati, binti mwenye ulemavu wa mwili ili ziweze kumsaidia kama mtaji wa biashara na uendelezaji wa ujenzi wa vyumba vya kupangisha katika nyumba ambayo amekabidhiwa leo (Ijumaa, Januari 22, 2021) na Waziri Mkuu. Gharama ya ujenzi wa nyumba na samani zilizomo ndani ni sh. milioni 47.32.

Waziri Mkuu ameendesha harambee hiyo kwenye kitongoji cha Fune, kata ya Mombo wilayani Korogwe baada ya kumkabidhi binti huyo nyumba aliyojengewa na wadau mbalimbali kutokana na mchango ulioasisiwa na Waziri Mkuu Machi 5, 2020 alipomtembelea Miriam na kumpatia mchango wa sh. milioni 5 za kuanza ujenzi wa nyumba hiyo.

Waziri Mkuu alimsaidia Miriam baada ya kumsikia binti akimuomba amsaide kupata makazi yeye na bibi yake kupitia kipindi cha Wape Nafasi kinachoongozwa na Tuma Dandi, mtangazaji wa Shirika la Utangazi Tanzania (TBC1).

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents