Habari

RC Chalamila: Mwalimu mkuu anafika shuleni saa mbili, nimemuuliza na division one ngapi ? (+ Video)

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila amemtaka Afisa Elimu wa Mkoa wa Mbeya, Majuto Njanga kufanya mabadiliko ya Mwalimu Mkuu wa Shule ya sekondari Iyela iliyopo Jiji la Mbeya kwa kushindwa kusimamia taaluma na nidhamu shuleni hapo.

RC Chalamila pamoja na kumtaka Afisa Elimu Mkoa kufanya mabadiliko ya uongozi katika shule ya Iyela, pia amemtaka Katibu Tawala wa Mkoa kufanya mabadiliko katika Shule zote ambazo mwenendo wa matokeo yake umeshuka mfululizo kwa miaka mitatu.

Chalamila ameyasema hayo akiwa katika kikao kazi cha kujadili mkakati wa taaluma mkoani hapo.

Bofya hapa kutazama.

https://www.instagram.com/tv/CKWp4QZBcZG/

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents