FahamuHabari

Tanzania namba moja kwa watu wenye unene Afrika Mashariki

Kunenepa sana sio tu kushindwa kuficha manyama uzembe au kutotosha kwenye nguo. Sasa ni janga la afya duniani ambalo linaonekana wazi lakini mara nyingi hupuuzwa. Watafiti wanasema kuwa unene kupita kiasi ni aina nyingine ya utapiamlo.

Utafiti mpya uliofanywa na shirika ya The Lancet unaonyesha kuwa kufikia mwaka 2022, zaidi ya watu bilioni moja duniani watakuwa na unene uliopita kiasi.

Data iliyokusanywa kutoka nchi 200 katika miongo mitatu iliyopita pia inaonyesha kuwa asilimia 43 ya watu wazima duniani wana uzito kupita kiasi.

Utafiti wa unene kupita kiasi, barani Afrika, kwa upande wa wanawake unaonesha kuwa ni nchi za Misri 59%, Libya 48%, Afrika Kusini 48%, Eswatini 45% na Ushelisheli 41% zinazoongoza kwa kuwa na watu wenye unene kupita kiasi.

Na kwa upande wa wanaume ni Misri 32%, Libya 28%, Ushelisheli 21%, Eswatini 16%, na Afrika Kusini 15%.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents