Michezo

Sababu ya mafanikio ya Yanga – Farhan Kihamu, Sehemu ya Kwanza

Mashabiki wa Arsenal walimtambua Boss wao ama Mmiliki wa timu yao Bilionea Stan Kroenke kama Tajiri asiyejua mpira na walimpa jina la utani kama ‘Silent Stan’ wakiamini hana alijualo kwenye mpira, kutokana na umri Baba ilibidi akubali na baadae akampa Kijana wake Josh Kroenke, aisimamie Arsenal! Ndio hii inayosumbua kwasasa.

Heshimu sana neno UMRI kwenye mpira wa miguu, umri mdogo huleta njaa ya mafanikio! Klabu ya Juventus ni mali ya familia ya Matajiri wa enzi familia ya Agnelli pale Italia ambao wanaishi milimani Villar Pellosa, wao waliona wampe Kijana wao Andrea Agnelli asimamie timu na alisumbua sana soka la Italia kabla ya kashfa kubwa.

Wakati Rais Perez anajiuzulu kwa mara ya kwanza kama Rais wa Real Madrid inatajwa alichukua maamuzi hayo baada ya project yake kufeli, ila aliporejea hakutaka tena kurudia makosa, alimpa kazi kijana kuwa CEO wa Real Madrid, Jose Angel Sanchez anapiga mzigo pale tangu 2009 hazungumzwi sana ile ndio kichwa nyuma ya Rais Perez.

Ndio huyu Jamaa ambaye amekuja kufanya kazi kubwa na Chief Scout Junior Calafat wamerejesha sera ya Zidane Y’Pavones na kuitupa rasmi sera ya GALACTICOS ambapo Don Perez alikubali, hili ni somo la siku nyingine kuhusu intergration ya soka la Vijana wa Castilla na Mastaa.

Ukiigusa Menejiment ya Real Madrid unagusa Wasomi wa daraja la juu na Wafanyabiashara, ili uwe Rais wa Real Madrid inabidi ukopesheke benki kama BILLION 100 na uwasilishe hati (means testing) kwa kifupi timu zote kubwa zilizofanikiwa hawataki Kiongozi njaa, unawasilisha mpango kazi wako kuhusu timu wakati unaomba ridhaa sio maneno tu.

SORRY nimeitumia picha ya Yanga kama mfano tu wa MENEJIMENT za Ulaya, kuna Wasomi humo, kuna Wafanyabiashara wakubwa na Matajiri, mfumo ambao klabu inachukua pesa zao na sio wao kuchukua pesa za klabu, lakini bado ni vijana damu changa, fuatilia klabu zote duniani wamejaza sura kama hizi, mpira ni BIASHARA sio hisani tena.

Nataka niwape kisa cha sakata la usajili wa Jude Bellingham kisha utaunganisha na sakata la usajili wa Aziz Ki hapa Bongo, nataka tuzungumze mpira kwa kuzigusa Simba na Yanga zote, lengo tujifunze na tuamke usingizini haswa SIMBA.

 

 

 

INAENDELEA….

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Imeandikwa na Mbanga B.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents