HabariTechnology

Waziri Nape ashiriki uzinduzi wa 5G kwa mara ya kwanza Tanzania

Kampuni ya Vodacom Tanzania imefanya uzinduzi rasmi wa kibiashara wa teknolojia ya 5G Tanzania na kuifanya Tanzania kuwa kati ya nchi chache za Afrika zenye teknolojia.

 

Uzinduzi huo wa kihistoria umefika leo Septemba 1, 2022, katika ukumbi wa matukio wa Mlimani City jijini Dar es Salaam ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mheshimiwa Nape Moses Nnauye.

 

Katika namna ya kuvutia sana iliyoibua shangwe ukumbini hapo, ilitangazwa kwamba kutokana na majukumu mbalimbali ya Kitaifa, Waziri Nape Nnauye ameshindwa kufika ukumbini kwa wakati hivyo akalazimika kutoa hotuba yake ya awali akiwa mbali na ukumbi huo, lakini teknolojia ya 5G ilimfanya aonekane kama yuko ukumbini hapo mfumo wa ‘hologram’ ikiwa ni mara ya kwanza kabisa Tanzania.

 

Kaimu Mtendaji Mkuu wa Vodacom, Hilda Bujiku, alieleza kwamba mfumo wa Hologram ukiwa na pande mbili (Double Hologram) ni wa kwanza Duniani.

 

Katika hotuba aliyotoa kabla ya kufika ukumbini, Waziri Nape Nnauye alisema ilikuwa ngumu kufikiri kama dunia ingefika katika hatua hii huku akiipongeza Vodacom kwa kuleta mapinduzi haya Tanzania. “Nakumbuka mwezi wa tano mwaka huu (2022), tuliahidi Bungeni kwamba Tanzania mwaka huu wa fedha itaanzisha  huduma ya 5G hapa nchini. Wakati ule tuliposema Ilikuwa kama ndoto, ‘now it is only three months’ (sasa ni miezi mitatu tu) toka tuliposema ‘Vodacom has made it’ (Vodacoma wametenda), wametusaidia kuingia kwenye orodha ya nchi chache kabisa Afrika ambazo zimeazisha huduma ya teknolojia ya 5G.” amesema Nape.

 

Baadae Waziri Nape Nnauye aliweza kufika katika ukumbi huo, na kuweza kutoa hotuba iliyojikita katika kuelezeza namna ambavyo 5G iliyoletwa na Vodacom itanufaisha nchi katika Nyanja zote akitolea mfano wa sekta za kilimo, nishati, elimu na afya.

“Serikali kupitia Wizara inaunga mkono kikamilifu sekta binafsi na mfumo wa teknolojia ya uvumbuzi kwa sababu tunajua kuwa teknolojia kama vile Mtandao wa Vitu (IoT), akili bandia (Artifial Intelligence), na kujifunza kwa mashine (Machine Learning), eknolojia ya blockchain, mtandao wa 5G, roboti, na kompyuta zinaongezwa katika kutoa masuluhisho na kusaidia nchi kufikia malengo yake ya SDG. Kwa hivyo, leo tunaunga mkono kikamilifu maendeleo haya tunapozindua rasimi kibiashara (market launch) teknolojia hii ya 5G hapa nchini na Upatikanaji wa mtandao wa kasi ukijulikana kama “Wireless ya Fibre” hii inadhirisha Kampuni ya Vodacom Tanzania inazidi kuongoza kuongoza katika ubunifu wa huduma na Teknolojia hapa nchini.” Amesema Nape.

 

Waziri Nnauye aliongeza “Teknolojia hii itakuwa na manufaa katika sekta zote za uchumi na kijamii nchini, hivyo kuleta maendeleo na mageuzi kwa watanzania wote hususan tukiangazia kupelekea Tanzania ya uchumi wa Kidigiti. Napenda kusisitiza hoja hii, Teknolojia mpya inayozinduliwa hapa leo itakuwa na nafasi ya kuleta mabadilikjo makubwa ambayo yataleta matokeo chanya katika nyanja nyingi za shughuli za kiuchumi na kijamii kulingana na matarajio ya nchi yetu ya kujenga Tanzania ya uchumi wa Kidijiti”

 

Naye Andrew Lupembe, Mkurugenzi wa Mtandao wa kampuni ya Vodacom, alieleza kwamba Vodacom inajivunia kuwa ya kwanza kutambulisha rasmi kibiashara mtandao wa 5G kuweka wazi kwamba wataweka zaidi ya vituo 200 vya 5G ndani ya Tanzania hadi kufikia mwezi Novemba, 2022.

 

Kutokana na mapinduzi hayo makubwa yaliyofanywa na Vodacom, Tanzania sasa inaungana na nchi za Botswana, Egypt, Ethiopia, Gabon, Kenya, Lesotho, Madagascar, Mauritius, Nigeria, Senegal, Seychelles, Afrika Kusini, Uganda, na Zimbabwe kuwa nchi chache za Afrika zenye teknolojia ya 5G.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents