Habari

Waziri wa Maji Jumaa Aweso, atinga DAWASA usiku na kutoa maagizo mazito

Waziri wa Maji, Juma Aweso ameongoza kikao usiku kucha cha mikakati na Menejimenti ya Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (Dawasa) ili kujadili suluhu ya muda mfupi na muda mrefu pamoja na kuwapa hamasa Watumishi katika kipindi hiki kigumu.

Aweso amewataka wataalam kutumia ubunifu na maarifa yao yote kuwasaidia wana Dar Es Salaam.

Pia amesisitiza watumishi wa Mamlaka kufanya kazi usiku na mchana na kuhakikisha migao ya maji inatolewa kwa uwiano na bila upendeleo.

Aidha ameitaka DAWASA kutoa bei elekezi kwa watoa huduma binafsi wa maji kupitia magari( bowsers).

Mwisho Aweso ameahidi ushirikiano wa Wizara katika kukabiliana na changamoto zilizopo kwa DAWASA na Bonde la Wami Ruvu.#Bongo5Updates

2 m

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents