Burudani

Mapacha wa P Square wamaliza tofauti zao (+ Video)

Habari kubwa kutoka Afrika tangu usiku wa kuamkia leo ni kwamba kundi la P SQUARE ambalo lilikuwa linaundwa na ndugu wawili Peter Okoye @peterpsquare na Paul Okoye @iamkingrudy limerudi ingawa bado haijaeleweka hata muziki wataanza kutoa pamoja au laah.

Hii ni baada ya usiku wa kuamkia leo kukutana kwa mara nyingine baada ya kutengana kwa miaka kadhaa, tofauti hizi ziliisha tangu wiki iliyopita alipoonekana @peterpsquare akiwachukua watoto wa kaka yake @iamkingrudy ambao wanaishi Marekani na kuwapeleka shopping.

Baada ya kuonana wanarudi kama mwanzo na ukiangalia kwenye video hapo @peterpsquare akisalimiana na kaka yake mkubwa ambaye ndio alikuwa meneja wao kwa furaha kubwa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents